Dar es Salaam. Kama ulijiandikisha na unatarajia kutumia kitambulisho chako kuwachagua wale wote ambao unawaona wanastahili kuwemo kwenye orodha ya viongozi wa serikali ya awamu ya tano na hutaki kukosea, usifanye mambo 12 yafuatayo:
1. Usijaribu kupiga kura zaidi ya mara moja.
2. Usijaribu kupiga kura baada ya muda kwisha.
3. Usijaribu kupiga kura kwa kutumia kadi ya mtu
mwingine.
4. Usiweke kitu kingine zaidi ya karatasi ya kupigia kura
katika sanduku la kuhifadhia kura.
5. Usichane orodha ya wapiga kura au mabango yoyote
ya elimu kwa mpigakura.
6. Usighushi au kuharibu karatasi ya kura.
7. Usichapishe na kusambaza karatasi za kura bila mam
laka kisheria.
8. Usipokee au kutoa rushwa kabla na wakati wa uchaguzi.
9. Usimzuie mwingine kupiga kura kwa uhuru na amani.
10. Usitoe siri ya kiongozi aliyepigiwa kura na yeyote.
11. Usiweke alama yoyote ya utambulisho katika karatasi ya kura.
12. Usivae au kuonyesha alama yoyote ya chama wakati wa
upigaji kura.
CHANZO MWANANCHI

0 comments:

 
Top