Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Mvumi jimbo la Mtera wilaya ya Chamwino leo wakati akiendelea na kampeni zake katika majimbo ya Isimani mkoani Iringa, Kibakwe na Mtera mkoani Dodoma, ambapo amewaomba wananchi hao kutohadaika na wagombea wanaowadanganya kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya kitu kwa miaka 54
Dk. Magufuli amesema kuwaambia watanzania CCM haijafanya kitu kwa miaka 54 ni jambo ambalo linachekesha kwani Utulivu na amani tuliyonayo ni matunda ya uongozi bora wa viongozi wa serikali ya CCM waliopita wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, “Wanapita kwenye barabara za lami zilizojengwa na serikali ya CCM tena nikizisimamia mimi John Pombe Magufuli, Wanatumia miundombinu ya mawasiliano na Umeme uliosambazwa kwa zaidi ya asilimia 40 nchini na serikali ya CCM lakini wanasema haijafanya kitu ni jambo la kushangaza.
Mbaya zaidi wamekuwa viongozi wa serikali tena wakiwa na nyazifa kubwa serikalini, sasa kama walishindwa kuwajibika na kuwatumikia watanzania wakiwa serikalini kwa nini hawakuondoka mapema, Lakini muda wote wakabaki CCM wakisifia mafanikio hayo ambayo leo wanayaponda. Si sawa kabisa hao wanatafuta madaraka kwa kutaka kuwadanganya watanzania nawaasa msikubali kudanganywa waongo hawa.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-MVUMI-DODOMA)
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Isimani mkoani Iringa Mh. Willliam Lukuvi katika mkutano uliofanyika kata ya Pawaga.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Mvumi mkoani Dodoma leo.
0 comments:
Post a Comment