Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewasili nchini Marekani kupinga dhidi uwezekano wa kufikia makubalino na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.

Bwana Netanyahu anasema mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.
 

Netanyahu anatarajiwa kulihutubia Bunge la Congress Jumanne, hotuba ambayo haikukubaliwa kabla na utawala wa Rais Obama na kuiudhi Ikulu ya Marekani.

Hotuba hiyo inakuja wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Israel, huku chama chake cha Likud kikiwa katika shinikizo katika uchaguzi wa nyumbani.

Marekani na mataifa mengine yanayotambulika kama P5+1 - wanajadiliana na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Wanataka mpango wa makubaliano kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambao unaeleza wasiwasi kuwa Iran inatafuta teknolojia ya silaha za nyuklia, jambo ambalo linakanushwa na Iran.
chanzo bbc

0 comments:

 
Top