Serikali
ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa
Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau.
0 comments:
Post a Comment