Jumuiya ya kieneo ya IGAD huko Afrika Mashariki imetangaza kuwa,
mazungumzo ya amani kati ya makundi hasimu kwenye mgogoro wa Sudan
Kusini yataanza tena wiki ijayo baada ya kuvunjika miezi miwili
iliyopita.
Taarifa ya IGAD imesema mazungumzo hayo yataanza siku ya Jumatatu mjini Addis Ababa, Ethiopia na kwamba upande wa serikali ya Sudan Kusini na ule wa waasi zimekubali kurudi tena kwenye meza ya mazungumzo. Mazungumzo hayo yalikuwa yamepangiwa kuanza tena wiki hii lakini yakaahirishwa kutokana na sababu za kisiasa.
Mwezi Juni mwaka huu mazungumzo ya amani kati ya ujumbe wa serikali ya Rais Salva Kiir na ule wa makamu wa zamani wa rais, Dkt. Riek Machar, yalivunjika huku kila upande ukiutuhumu upande wa pili kuwa ndio uliosababisha kuvunjika kwa mazungumzo hayo.
Mashirika ya kutoa misaada ya chakula pamoja na Umoja wa Mataifa zimetahadharisha kuwa, baa kubwa la njaa linaweza kutokea Sudan Kusini endapo mapigano yataendelea kushuhudiwa.
Chanzo Radio tehrani

0 comments:
Post a Comment