Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema stratijia
ya Jamhuri ya Kiislamu ni kufuatilia amani na uadilifu duniani, na
katika ulimwengu wa Kiislamu ni kufuatilia umoja.
Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo Jumanne mjini Tehran katika mkutano wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na maafisa wa ngazi za juu nchini, mabalozi na wawakilishi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbali mbali kwa mnasaba wa Siku Kuu ya Idul Fitr.
Akihutubu katika baraza hilo la Idul Fitr, Rais Rouhani ameongeza kuwa, katika Ulimwengu wa Kiislamu, Iran inataka kuona udugu, umoja, mshikamano na juhudi za kuunda umma moja wa Kiislamu.

Rais wa Iran amebainisha masikitiko yake kuwa, katika eneo na katika
Ulimwengu wa Kiislamu kuna vivimbe viwili sugu vya saratani; amesema cha
uvimbe wa kwanza ni ule ambao umewapelekea Wapalestina na Waislamu
wapate uchungu mkubwa na katika siku za hivi karibuni umepelekea
umwagikaji mkubwa wa damu ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
Rais Rouhani ameendelea kusema kuwa uvimbe wa pili sugu wa saratani ni ule ambao umepelekea Waislamu wapate masaibu katika siku za hivi karibuni kupitia ile harakati ambayo imeanza kwa jina la Uislamu, dini, ukhalifa na imarati na kuanza kuwaua Waislamu na wasio kuwa Waislamu katika eneo.
Amesema tathmini zinaonyesha wazi kuwa vivimbe hivi viwili vya saratani vinatoka sehemu moja. Rais Rouhani amesema njia pekee ya kutatua matatizo hayo ni umoja wa nchi za Kiislamu.
Amesema nchi za Kiislamu duniani zinapaswa kuwa zenye kutoa wito wa amani na uadilifu duniani huku zikiwasilisha muongozo wa kujiweka mbali na ujahili au ujinga na taasubu.
Rais Rouhani pia ametoa wito wa kuandaliwa mazingira ya kufikishwa katika vyombo vya sheria watenda jinai katika utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari hii imeandaliwa kwa msaada wa vyombo vya habari vya Irani.

0 comments:
Post a Comment