HABARI ZA MITANDAONI ZISIWEKE MAISHA YA WATANZANIA REHANI
Habari mitandaoni kupitia blogs,a mitadao ya kijamii zimekuwa mkombozi vyanzo muhimu vya habari kutokana na ufanisi na uwezo wake wa kufikisha habari toka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania kwa haraka na muda muafaka uwezo ambao vyombo vya habari kama Radio,Televisheni pamoja na magazeti havina.
Aidha vyombo hivi vimekuwa mkombozi kutokana na kukosekana kwa sheria ya moja kwa kwa moja ya kuvibana vyanzo hivi vya habari kama ilivyo kwa sheria za magazeti na vyombo vya utangazaji yaani Radio na Televisheni hali inayovipa nafasi vyanzo hivi vya habari kuwa huru katika utoaji wa habari ambazo Radio na Televisheni na magazeti  zisingeweza kutoa kwa kuofia kwenda kinyume na sharia zinazoogoza vyombo hivyo.
Uhuru huu wa habari za mitandaoni wakati mwingine  umekuwa ukitumika vibaya na baadhi ya watu kwa kuanzisha mitandao iliyojaa picha za ngono,stori za maisha ya watu ,video za ngono huku mambo yenye tija kwa jamii  kama vile elimu ya kilimo bora,bei za bidhaa masokoni,taarifa za hali ya hewa zinazohitajika na wakulima katika sughuli za kilimo zikinyimwa nafasi.
Dhana ya habari kwamanufaa ya umma imepuuzwa kinachotazamwa sasa ni kipi kinapendwa zaidi na jamii kwa lengo la kupata matangazo kutokana na kuwa na wafuatiliaji wengi dhana hii haipaswi kuungwa mkono hata kidogo.Tusikubali mustakabari wa maisha ya watazania yakachezewa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi.
Imekuwa ni kawaida sana kwa blog za watanzania kujaa story zinazohusu maisha binafsi ya watu,picha za uchi,habari za chuki,kuchafuana,unafiki ili mradi mtu amejisikia kuweka habari ianayomjia kichwani mwake bila kujali imani kubwa iliyopewa mitandao hiyo.
Jambo kubwa la kusikitisha mitandao hiyo yenye habari,picha na video chafu kuwa na wapenzi wengi vijana wakiwa wengi zaidi,hali hii inasikitisha sana,wapi tunalipeleka taifa hili,nini mustakabali wa maisha ya vijana wa kitanzania,vizazi vya namna gani tunaviandaa.Sina lengo la kuunga mkono moja kwa moja uthibiti wa matumizi ya mtandao lakini kwa hali hii ipo haja ya udhibiti wa matumizi wa mitandao kwa manufaa ya umma.
Tumeziona jitihada mbalimbali zilizofanywa na Tume ya udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).Ikiwemo uendeshaji wa semina na warsha mbalimbali kwa wamiliki wa blog lengo likiwa ni kusisitika matumizi sahihi ya mitandao kwa mustakabali wa taifa.
Aidha kampeni mbalimbali zinafanywa kusisitiza matumizi mzuri ya mitandao kukifuatiwa na kauli mbiu mbalimbali kama vile ukiona ujumbe wa chuki,uchochezi na uongo futa delete kabisa ili mradi tu kuhakikisha uhuru wa habari mitandaoni unatumiwa vyema.
Licha ya jitihada hizo bado tatizo la matumizi mabaya ya mitandao linashamiri hususani uwepo wa picha zisizofaa mitandaoni,habari za uongo udaku ukitawala na huku mambo ya msingi kwa maendeleo ya watu a taifa kwa ujumla kutopewa kipaumbele.
Kwa mantiki hii ipo haja sasa ya kusajili, kutoa mafunzo ya kimaadili na kitaaluma kwa wamiliki wa blog nchini ili blogu hizo zilete mchago chanya kwa maendeleo ya Taifa hili na si wao kuwa chanzo cha kuporomosha maadili ya vijana wetu,kusababisha chuki na mengineyo mengi.

0 comments:

 
Top