UWINDAJI HARAMU WA NDOVU WAENDELEA KUITESA KENYA
Pembe za ndovu katika picha
Maafisa hao wameelezea kuwa wakuu wamenasa zaidi ya pembe 1,600 za ndovu katika juma moja lililopoita.Mzigo mmoja wa pembe hizo uliokuwa uzani wa kilo 1900 ulinaswa Ijumaa mjini Mombasa.
Pembe hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya mbegu za Sim Sim zilizokuwa ndani ya magunia zikiwa safarini kwenda Uturuki.
Aidha Pembe zengine zenye tani mbili zilinaswa kwenye bohari lengine.
Kuongezeka kwa uwindani haramu kumekita mizizi katika maeneo ya Kusini mwa jangwa la Sahara ambako makundi ya wahalifu wenye siasa wanawaua Ndovu kwa ajili ya soko la pembe zake na Vifaru ambazo hutumiwa kama dawa barani Asia.
Baadhi ya pembe ziliingizwa Kenya kupitia mpaka wa Uganda na Kenya na zilikuwa zimefichwa ndani ya mabohari mawili.
Stakabadhi za wenye mizigo zilionyesha kuwa mabohari hayo yalikuwa yamebeba mbegu za Sim Sim.
Pembe hizo zilipatikana katika matukio mawili mabli mbali na zilisemekana kuwa na thamani ya dola milioni 1.14, kikiwa kiwango kikubwa cha Pembe za Ndovu kukamatwa katika miaka mitano iliyopita.
Afisaa mmoja wa forodha alisema kuwa wawindaji haramu wamekuwa na uzoefu wa kusafirisha pembe hizo kupitia nchi ambazo kawaida hazijahusishwa na biashara ya pembe za Ndovu ili kufumba macho ya maafisa wakuu.
Hata hivyo Maafisa wa nchi hiyo watafanya uchunguzi wa DNA kujua ambako pembe hizo zimetoka.
0 comments:
Post a Comment