PATA ELIMU HAPA
Kuharamisha
Kuingilia Katika Tupu ya Nyuma
Allah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Amesema:
“ Wake zenu ni konde zenu, basi ziendeeni
konde zenu mpendavyo.” (Baqara: 223)
Ilikuwa ni tabia ya
Mayahudi wakisema: Mtu atakapomuingilia mke wake mbele lakini kwa upande wa
nyuma basi atazaliwa mtoto akiwa ni kengeza; ikashuka aya hii: “Wake zenu ni mashamba
yenu.” (Muslim).
Katika
riwaya nyingine:
“…na ukipenda ufanye staili ya kama anasujudu na ukipenda sivyo hivyo yote ni sawa
sawa...” (Muslim: Hadithi 1435)
Ilikuwa ni tabia ya ahlul
kitaab kutomuingilia mwanamke ila kiubavu na katika hali ya mwanamke
kujistiri. Na ilikuwa tabia ya baadhi ya Ansaar kuiga tabia zao hizo. Na
wanaume wa ki-qureish walikuwa wamezowea kufanya mapenzi na wake zao vilivyo,
wakistarehe nao kwa mbele, nyuma na kwa chali, (lakini bila ya kuwaingilia tupu
zao za nyuma). Walipohamia Muhajirina Madina alioa mmoja wao mwanamke wa
ki-ansaar; akataka kufanya nae mapenzi kwa mitindo waliyozoea (huko Makka)
akachukizwa mwanamke yule na hilo,
na akasema: Hakika sisi tulikuwa tukiingiliwa kiubavu, fanya hivyo au niepuke;
kisa chao kikaenea, zikamfikia habari Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam)
na Mwenyezi Mungu Akashusha:
14
“Wake zenu ni konde zenu…” (Abu Daud)
Na Mtume (Swalla Llaahu
'alayhi wa sallam) akasema vile vile:
“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo
wa)Kwa mbele au (kwa mtindo wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (mkundu) na
(kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.” (Tirmidhi)
0 comments:
Post a Comment