![]() |
Hayati Nelson Mandela |
Nelson Mandela ameaga dunia.
Mandela
amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza
Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya
kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela
alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini
kwa miezi mitatu.
Katika
taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela
amewaaga lakini yuko mahali salama.
Mnamo
mwaka 2005, Mandela aliushangaza umma baada ya kutangaza hadharani kuwa mwanawe wa kume alifariki
kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Rais
Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela
aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais
aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya
kuondoka gerezani.
Hakuonekana
sana hadharani tangu alipostaafu mwaka 2004.
chanzo bbc
0 comments:
Post a Comment