Viongozi kutoka Afrika mashariki wanatarajia
kukutana nchini Kenya kujadili kuhusu machafuko yanayokithiri nchini Sudani
kusini, ambapo zaidi ya Watu 1,000 wanaaminika kupoteza maisha.Mazungumzo hayo
yanakuja siku moja baada ya Rais wa Sudani kusini Salva Kiir kukutana na
Mawaziri wakuu kutoka nchini Kenya na Ethiopia.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa kikosi
cha kwanza cha kulinda amani kinatarajiwa kuwasili nchini Sudani kusini saa
kadhaa zijazo.machafuko yalijitokeza siku 12 zilizopita kati ya vikosi
vinavyomuunga mkono Kiir na vile vinavyomuunga mkono aliyekuwa naibu wa Kiir,
Riek Machar. Zaidi ya raia 50,000 wamekimbia makazi yao na kuomba hifadhi
katika Ofisi za UN huko Sudani kusini.
Viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki kutoka jumuia
ya Igad watakutana jijini Nairobi kwa ajili ya kujadili maswala yaliyogusiwa
katika mazungumzo yaliyofanyika siku ya Alhamisi kati ya Rais Kiir na Viongozi
hao jijini Juba.
Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Habari wa Sudani
kusini Makuei Lueth ameliambia shirika la habari la AP kuwa mpaka sasa hakuna
mawasiliano na Machar.
Sudani kusini imekuwa ikipigania kupata Serikali
thabiti tangu kupata uhuru wao mwaka 2011, baada ya kujitenga.
CHANZO BBC/SWAHILI
0 comments:
Post a Comment