WACHEZAJI wa kigeni wa Simba, wamegoma kwenda mjini Songea kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Majimaji itakayochezwa keshokutwa Jumatano.
Kikosi cha Simba kimeondoka leo asubuhi kwenda Songea kikiwa na wachezaji 13 pekee huku ‘Maproo’ hao wakibaki jijini Dar es Salaam wakitaka kwanza walipwe mishahara yao ya mwezi uliopita.
Wachezaji hao ni kipa Vincent Angban (Ivory Coast), mabeki Emery Nimubona (Burundi), Juuko Murshid (Uganda), viungo Justice Majabvi (Zimbabwe), Brian Majwega (Uganda), Hamisi Kiiza (Uganda) .
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara, aliuambia mtandao mmoja wa soka kwamba sababu ya kuchelewa kuwapa mishahara wachezaji wao inatokana na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuchelewa pia kuwapatia fedha za udhamini.
Pamoja na waliogoma, Manara amesema Raphael Kiongera, Jonas Mkude, Awadhi Juma na Ibrahim Hajib nao hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa majeruhi na kutumikia adhabu za kadi.
Simba inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58 imekwenda Songea ikiwa imetoka kupoteza mechi yake dhidi ya Mwadui iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa na kufungwa bao 1-0.

Pamoja na waliogoma, Manara amesema Raphael Kiongera, Jonas Mkude, Awadhi Juma na Ibrahim Hajib nao hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa majeruhi na kutumikia adhabu za kadi.