MAWAZIRI WATEULE
WAREJESHE IMANI YA WATANZANIA DHIDI YA SERIKALI
Siku chache tu
zimepita tangu kuenguliwa kwa mawaziri wanne wa serikali ya jamuhuri ya
muungano wa Tanzania kutokana na
kushindwa kuisimamia vyema watendaji
katika operesheni tokomeza ujangili hali iliyopalekea ukiukwaji mkubwa wa haki
za binadamu ikiwemo mauaji pamoja na udharilishaji wa kijinsia uliosadikika
kufanywa na watendaji wa operesheni hiyo.
Mawaziri ambao
Rais alitengua kuendelea kusimamia wizara zao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, bwana
David Mathayo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, bwana
Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, bwana Emmanuel Nchimbi
na aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki.
Hata hivyo,
uamuzi wa Rais kuwaondoa mawaziri hao wanne hautakuwa na tija kama hawataondolewa
pia viongozi wa Vyombo vya Dola ambavyo vimelaumiwa na wabunge kwa kuhusishwa
na uvunjaji wa haki za binadamu uliojitokeza katika operesheni tokomeza ujangili.
Serikali pia
inapaswa kuwashughulikia Makatibu Wakuu wote na wakurugenzi wao wa Wizara nne
husika, pamoja na ile inayosimamia Utawala Bora, Wizara ambayo pia inasimamia
Usalama wa Taifa kwai wao pia ni sababu kubwa ya madhra yaliojitokeza kwenye
operesheni tokomeza ujangili.
Hata hivyo
serikali pia inapaswa kuchunguza kwa kina yale ambayo yamekuwa yakiendelea,
hususan katika Wizara ya Mali asili na Utalii, hasa katika eneo la vitalu vya
uwindaji na kadhalika. Kumekuwa na madai lukuki ya rushwa katika eneo hili!
Serikali ya
Raisi Kikwete imaevunja rekodi yakufanyika kwa mabadiliko ya mara kwa mara
kwenye baraza la mawaziri kutokana na uwepo wa watendaji wasiowajibika hali
inayopelekea hasara pamoja na maafa kwa Taifa .
Ikumbukwe
mabadiliko ya baraza la mawaziri yalianza mwaka 2008 baada ya kuvujwa kwa baraza
la mawaziri kutokana na kujiudhuru kwa aliyekuwa waziri mkuu bwana Edward
Lowasa kulikosababishwa na kashfa ya Richmond kulikofuatiwa na kujiuzuru kwa
aliyekuwa waziri wa nishati na madini Dk.Ibrahim
Msabaha kutokana na kashfa ya Richmond .
mabadilko
mengine ni Nazri Karamagi alingolewa kashfa ya Buzwagi,Ezekiel Maige alingolewa
kashfa ya twiga,Mustafa Mkulo wa wizara ya fedha aling’olewa kashfa ya
kiwanja,Dk.Haji Mponda alingolewa mgomo wa madaktari,William Ngeleja
alienguliwa kashfa ya umeme pamoja na mabadiliko megine mengi.
Kitendo cha
Raisi kuwavua nyadhifa mawaziri hao
kimesaidia kuiokoa
serikali yake dhidi ya kupigiwa kura na wabunge ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu wake hatua ambayo ingempelekea Rais kuvunja serikali yake au yeye mwenyewe
kupigiwa kura hiyo na hivyo kulipeleka taifa katika uchaguzi mkuu wa kuchagua
serikali nyingine.
Aidha baada ya kueguliwa
kwa mawaziri hao wanne watanzania wanasubiri kwa hamu
wateule wapya wa nafasi zilizowazi kwa imani ya kuwa wateule hao watakwenda
kusafisha uozo ulioko kwenye wizara hizo kwa kuwawajibisha watendaji mizigo,wabadhilifu
na wabinafsi ndani ya wizara hizo na kurudisha heshima na imani ya watanzania
iliyotoweka kwa sasa.
Watanzania pia
wanategemea kuona watendaji waliosababisha madhara kwa kukiuka haki za
kibinadamu vikiwemo vyombo vya dora wanashuhurikiwa kwa mujibu wa sheria na
taratibu za nchi na si kuishiakuvuliwa nyadhifa kwa mawaziri.
Naamini imani ya
watanzania dhidi ya baadhi ya watendaji wa serikali itarejea pindi hatua za
makusudi dhidi ya watendaji wadhembe zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na
kuwafukuza kazi na kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwashtaki
ili iwe funzo kwa wengine katika utendaji wao.
0 comments:
Post a Comment